Home Soka Simba Sc Yapangwa na waarabu Caf

Simba Sc Yapangwa na waarabu Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imepangwa katika kundi A la michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika katika droo iliyofanyika nchini Misri katika makao makuu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (caf).

Droo hiyo iliyofanyika majira ya mchana wa Oktoba 7 jijini Cairo ilishuhudiwa klabu ya Simba Sc ikiangukia katika kundi A likiwa sambamba timu za Cs Sfaxien ya nchini Tunisia na Cs Constantine ya Algeria pamoja na klabu ya Onze de Marquiz ya nchini Angola.

Kutokana na kupangwa kwa makundi hayo,Ratiba kamili inaonyesha kuwa klabu hiyo itaanzia nyumbani dhidi ya Onze de Maquiz siku ya tarehe 27 mwezi Novemba kisha itasafiri kuelekea nchini Algeria kuvaana na Cs Constantine Disemba 8 na kisha itarejea nchini kuwakaribisha Cs Sfaxien ya Tunisia wiki moja baadae.

banner

Ili kufuzu hatua ya robo fainali pamoja na kundi hilo kuonekana kuwa rahisi kwa Simba sc basi haina budi kushinda michezo yote ya nyumbani ili kujihakikishia alama tisa kwanza huku ugenini ikicheza kimkakati zaidi.

Tayari baadhi ya wadau wa soka nchini wameona kama kundi hilo ni jepesi hasa wakiangalia historia ya klabu hiyo kwa miaka ya nyuma ilipokua bora kupita sasa hivi ambapo ilikua imeshuka sana na sasa inaanza kurejea taratibu japo haijafikia ule bora wa miaka hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited