Site icon Sports Leo

Simba Sc Yasaka Kipa Mpya

Klabu ya Simba SC inafikiria kumrudisha tena golikipa Ayoub Lakred kurudi kuitumikia klabu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya kutoridhishwa na kiwango cha kusuasua cha kipa Moussa Camara.

Mpaka sasa suala hilo viongozi wa klabu hiyo wanasubiri ripoti rasmi ya benchi lao la ufundi ikiwa litamuhitaji Ayoub Lakred watamrudisha kikosini kuchukua nafasi ya Camara ambaye pia ameonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo.

Pia Simba SC inamfatilia kwa ukaribu sana golikipa wa Al Hilal ya Sudan, Issa Fofana ambaye amekuwa na msimu bora sana endapo itashindwa kupatana na Lakred inaweza kumsajili kipa huyo asaidiane na Salim langoni hapo.

Simba sc ilimtoa Lakred kwenye usajili wake msimu uliopita baada ya kipa huyo kuumia haloi iliyomlazimu kukaa nje ya uwanja akijitibia muda mrefu

Exit mobile version