Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi muhimu kuelekea katika hatua ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuifunga Nyasa Big Bullets kwa mabao 2-0 ugenini katika uwanja wa Bingu nchini Malawi.
Katika mchezo huo ambao Simba sc ilianza na mshambuliaji mmoja Moses Phiri aliyesaidiwa na mawinga Pape Sakho na Kibu Dennis iliwachukua Simba sc dakika 29 za kipindi cha kwanza kupata bao lililofungwa na Moses Phiri aliyepokea pasi ya Kibu Dennis na kufunga kwa Tiktaka baada ya mabeki wa Nyassa kuzubaa kuokoa mpira huo.
Wenyeji walijitahidi kusawazisha bao hilo lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Simba sc ikiongozwa na Henock Inonga na Mohamed Outara ulifanya kazi nzuri ya kuzuia mashambulizi ya wenyeji huku pia Simba sc ikifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 80 likifungwa na nahodha John Bocco na kuwamaliza nguvu wenyeji ambapo mpaka mpira unaisha Simba sc iliibuka na ushindi huo muhimu ugenini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana hapa nchini ambapo Simba sc atakua mwenyeji na matokeo ya jumla ndio yataamua nani anafuzu hatua ya pili ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.