Msafara wa mastaa wa klabu ya Simba Sc umewasili salama katika mkoa wa Arusha mapema leo kulekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Coastal Union.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utachezwa majira ya saa kumi jioni katika uwanja huo huku timu zote mbili zikiwa zimejipanga kuibuka na ushindi.
Katika msafara uliowasili mapema asubuhi ya leo wachezaji Moussa Camara na beki Che Malone Fondoh hawakuonekana katika msafara huo na kuendelea kuzua hofu pengine wanaweza kuukosa mchezo huo.
Wachezaji hao hawakuwepo mazoezini katika siku ya alhamis jioni katika uwanja wa Mo Arena Bunju jijini Dar es Salaam ambapo waliumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa sare ya 2-2.