Home Makala Simba sc Yatua Bondeni Kibabe

Simba sc Yatua Bondeni Kibabe

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imewasili kibabe nchini Afrika ya kusini kuelekea katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaofanyika nchini humo siku ya Jumapili saa moja usiku.

Mchezo huo wa marudiano umekua na presha kubwa kwa pande zote mbili huku ushindi wa 1-0 ilioupata Simba sc katika mchezo wa raundi ya kwanza ndio ukiwapa jeuri mjini na kujiamini wanaweza kupata sare ama ushindi utakaowavusha kwenda hatua ya nusu fainali ya kombe hilo la pili kwa ukubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.

Simba sc itaingia na faida ya kurejea kwa Sadio Kanoute na Joash Onyango ambao waliukosa mchezo wa awali uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na kuwa majeruhi huku Orlando wakiendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji kama Gabadino Mhango ambaye hana maelewano mazuri na kocha wake.

banner

Simba sc baada ya kuwasili ililazimika kutumia msafara wa balozi wa Tanzania nchini humo baada ya  maafisa wa Orlando Pirates kutowaandalia msafara wa polisi ili kuepuka foleni wakielekea hotelini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited