Home Soka Singida Big Stars Vs Yanga sc Kupigwa Zanzibar

Singida Big Stars Vs Yanga sc Kupigwa Zanzibar

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Singida Black Stars imeamua kuupeleka mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc katika uwanja wa Amaani Visiwani Zanzibar ili kupisha ukarabati unaoendelea katika uwanja wake wa nyumbani wa Ccm Liti.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Visiwani humo siku ya Oktoba 30 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni za ligi kuu nchini,Klabu zinaruhusiwa kucheza michezo miwili ya nyumbani nje y viwanja vyao vya nyumbani ambapo wanapaswa kutoa taarifa ya maandishi mapema kabisa.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto kutokana na ubora mkubwa Black Stars ambao msimu huu wameboresha kwa kiasi kikubwa kikosi chao chini ya kocha Patrick Aussems.

banner

Singida Black Stars mpaka sasa imefikisha alama 16 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kucheza michezo sita huku Yanga sc ikiwa katika nafasi ya nne alama 12 baada ya kucheza michezo minne ya ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited