Site icon Sports Leo

Soulymane Wa Montpellier Astaafu Soka

Veterani wa Montpellier na mshambuliaji wa zamani wa Senegal ,Souleymane Camara mwenye umri wa miaka 37 amebainishwa na Rais wa klabu ya Montpellier, bwana Laurent Nicollin kuwa mwanasoka huyo kastaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu 13.

Tangu ajiunge na Montpellier Souleymane mwaka 2008 kwa mkopo wa Jumla kutoka Nice, amefanikiwa kucheza mechi 335 na kuifungia mabao 58 klabu hiyo na hata kushinda taji la Ligue 1 msimu wa 2012 .

Exit mobile version