Home Soka Sowah Njiani Kutua Singida Black Stars

Sowah Njiani Kutua Singida Black Stars

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Jonathan Sowah yupo mbioni kujiunga na timu ya Singida Black Stars inayoshiriki ligi kuu ya Nbc nchini ambapo mpaka sasa dili hilo liko mbioni kukamilika.

Sowah mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Medeama Fc ya nchini kwao Ghana ambapo alijiunga na klabu ya Al Nasser ya Libya ambapo sasa klabu hiyo imekubali kumuuza kwa dau la zaidi ya shilingi laki mbili za Kitanzania.

Mpaka sasa dili hilo lipo mbioni kukamilika na staa huyo tayari amewasili nchini kukamilisha mazungumzo ikiwemo maslahi binafsi na anatarajiwa kutambulishwa rasmi wakati wa dirisha dogo la usajili litakalo funguliwa Disemba 15 mwaka huu.

banner

Sowah aliwahi kuhitajika nchini na klabu ya Yanga sc lakini dili hilo halikukamilika kutokana na sababu mbalimbali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited