Home Makala Staa Ajiondoa Tp Mazembe

Staa Ajiondoa Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa ushambuliaji raia wa Congo DR Màrcel Ngimbi Vumbi (27) ametuma barua kwenda kwa uongozi wa klabu yake ya Tp Mazembe akiomba kuvunja mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ili awe mchezaji huru.

Ngimbi ambaye aliwahi kuhitajika na vilabu vya Yanga sc na Simba sc za hapa nchini miaka michache iliyopita amekua na wakati mgumu klabuni hapo kutokana na hali ngumu ya klabu hiyo kiuchumi.

banner

Mbali na staa huyo pia staa mwisho Oscar Kabwit naye amesusia mazoezi na michezo ya klabu hiyo akishinikiza kulipwa madam yake mbalimbali klabuni hapo.

Tp Mazembe imekua na wakati mgumu kiuchumi tofauti na miaka ya nyuma kutokana na bosi wa klabu hiyo Moise Katumbi kujiingiza katika masuala ya siasa nchini humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited