Site icon Sports Leo

Staa Simba Sc Apata Dili Nono Hispania

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Jean Charles Ahoua amepata ofa nono kutoka klabu ya Armelia Fc inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania.

Mabosi wa klabu hiyo baada ya kuona video za michezo mbalimbali ya klabu ya Simba Sc anayoichezea mchezaji huyo wameridhika na uwezo wake na tayari wamefungua mazungumzo na menejimenti inayomsimamia mchezaji huyo.

Hata hivyo menejimenti hiyo imesema kuwa haiko tayari kwa sasa kujadili dili hilo mpaka mwishoni mwa msimu huu 2024-2025.

“Tayari klabu hiyo imevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na wapo tayari kuanza mazungumzo ya kumsajili lakini sisi mpaka sasa hatuko tayari mpaka msimu uishe ndo tutaanza kuangalia ofa”,Alisema mmoja ya mabosi wa menejimenti ya mchezaji huyo

Ahoua amekua na msimu mzuri klabuni hapo akifunga mabao 15 mpaka sasa na akisaidia upatikanaji wa mabao saba mpaka sasa katika ligi kuu ya Nbc pekee.

Exit mobile version