Home Makala Stars Mtegoni Afcon 2024

Stars Mtegoni Afcon 2024

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania imeingia katika mtego mzito kufuatia kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Ivory Coast mwezi Januari mwakani baada ya kupangwa kundi F lenye timu za Morocco,Congo Drc na Zambia.

Stars imeingia mtegoni kutokana na ukweli kwamba kundi hilo halitabiriki kutokana na timu hizo alizopangwa nazo kusheheni mastaa wanaocheza barani ulaya ukilinganisha na wale waliopo Stars ambao wengi wanacheza ama hapa nchini au barani Afrika kwa kiasi kikubwa.

Wakati Taifa Stars ikijivunia uwepo wa Mbwana Samata na Novatus Dismass ambao wanacheza timu kubwa barani humo,Zambia watakua na mastaa kama Patson Daka,Fashion Sankala anayeichezea Glagow Rangers,Lameck Banda anayeichezea Lecce inayoshiriki ligi kuu ya Seria A huku Drc Congo na Morocco zikiwa na mastaa kibao katika ligi kubwa za Uingereza,Italia,Hispania,Ufaransa na Ujerumani.

banner

Staa wa Taifa Stars anayeichezea klabu ya JS Kablie ya Algeria na Stars Simon Msuva amesema “Wachezaji tayari tuna uzoefu na mashindano hayo na timu hizi mbili tunazijua tuliwahi kucheza nazo kikubwa ni sisi kwenda kupamabana.”

Taifa Stars haina budi kukaza kamba ili kupata nafasi ya kufuzu hatua za 16 bora na kuendelea kutokana na ugumu wa wapinzani hao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited