Klabu ya Tabora United imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Namungo mchezo wa ligi kuu ya NBC uliochezwa leo Agosti 25,2024 katika uwanja wa Majaliwa ulioko wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Namungo ilitangulia kwa bao la kwanza lililofungwa na Mcongomani Djuma SShabani kwa penati kabla ya Heritier Makambo kuchomoa pia kwa penati na dakika za mwishoni mwa mchezo alitoa pasi ya goli kwa Salum Chuku aliyefanikiwa kufunga bao la ushindi.
Huo ni mchezo wa pili kwa Tabora United msimu huu ambapo mchezo wa kwanza walifungwa 3-0 na Simba ilhali Namungo ni mchezo wa kwanza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tabora United baada ya kumaliza michezo ya ugenini sasa itacheza mechi zake tatu mfululizo katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi dhidi ya Kagera Sugar,Prisons na Fountain Gate.
