Site icon Sports Leo

Tff Yaanza Vizuri Msimu Huu

Shirikisho la soka Tanzania(TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Group Six International wenye thamani ya zaidi ya bilioni 9 kwaajili ya ujenzi wa vituo viwili vya ufundi ‘Techinical centre’ vilivyopo Tanga na Kigamboni.

Vituo hivyo vwili vya ufundi vitakua na viwanja visivyopungua vitatu kwa kila kituo pamoja na  hosteli za kisasa ndani yake.

Ujenzi wa miradi hiyo unategemewa kuanza mapema mwezi wa 10, ambapo itajengwa yote kwa pamoja kwa awamu mbili na kutegemewa kumalizika ndani ya kipindi cha miezi 12,kwa maana ya mwaka mmoja.

Exit mobile version