Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17 imeibuka na ushindi mnono wa mabao 10-0 dhidi ya timu ya Zimbabwe katika michuano ya Cosafa inayofanyika nchini Afrika ya Kusini.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Mohame aliyetupia mabao mawili dakika ya 18 na 89 huku mengine yakifungwa na Protasia Kipaga dakika ya 1,Koku Kipanga dakika ya 11, Irene Kisisa dakika 13, Ester Mabaza dakika ya 32.
Zawadi Athuman dakika ya 55, Asha Masaka naye alitupia mawili dakika ya 71 na 82, Rudo Machadu alitupia dakika ya 79 kwa upande wa Zimbabwe na kufanya liwe bao lao pekee la kufutia machozi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tanzania sasa imeingia katika hatua na fainali na inatarajiwa kumenyana na Zambia leo novemba 11 katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu na wenye msisimko.