Home Makala Urais Yanga sc Washika Kasi

Urais Yanga sc Washika Kasi

by Sports Leo
0 comments

Huku ikiwa leo Juni 9 ndio mwisho wa kuchukua fomu za kugombea urais katika klabu ya Yanga sc tayari vigogo mbalimbali wamejipanga kuchukua fomu hizo kuwania nafasi hiyo mpya klabuni hapo katika uchaguzi utakaofanyika Julai 10 mwaka huu.

Nafasi hiyo imeonekana kuwavutia vigogo wengi ndani ya klabu hiyo huku ikisemekana Eng.Hersi Said,Abbas Tarimba,Seif Magari,Davis Mosha na mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo Dk.Mshindo Msola tayari wameonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo na wanaweza kuchukua fomu muda wowote kuanzia hivi sasa.

Pia Dk.Athuman Kihamia ambaye ana nafasi kubwa serikali nae pia ameonyesha nia ya kuutaka Urais huo huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakimpigi debe Eng.Hersi kugombea kwa maana anakubalika ndani ya klabu hiyo kutokana na mabadiliko makubwa ya kikosi aliyofanya katika usajili wa wachezaji msimu huu.

banner

Yanga sc inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mwezi Julai mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa katiba mpya ambayo imeleta mabadiliko ya Uongozi ndani ya klabu hiyo kutoka kuwa na mwenyekiti mpaka nafasi ya Urais pamoja na wajumbe kadhaa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited