Bodi inasimamia ligi kuu soka nchini Uingereza(Premier league) imekaa ombi la vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo kuvaa jezi za ugenini katika mechi za nyumbani kama sehemu ya kuchangia watu wasio na makazi.
Vilabu vya ligi hiyo vilipanga kufanya hivyo tarehe 25-26 mwezi Desemba kipindi cha sikukuu ya Christmass.
Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo imesema kuwa kuchangia watu wenye mahitaji mbalimbali ni jambo jema lakini ni lazima lifanyike kwa kufuata sheria na kanuni zinazosimamia ligi na si vinginevyo.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi ya Uingerza timu ya nyumbani hazirusiwi kuvaa jezi tofauti na zile zilizoainishwa kisheria kutumika katika michezo ya nyumbani.
No home kit ni programu iliyoandaliwa maalumu kuonyesha ukubwa wa matatizo ya kukosa makazi yaliyosababishwa na janga la Uviko-19 nchini humo ambapo watu zaidi ya 180,000 wameachwa bila makazi.Ombi hilo lilipelekwa kwa vilabu vitakavyocheza nyumbani siku ya Boxing Day ambapo ingehusisha kuvaa jezi za ugenini kwa wacezaji na mashabiki kuonesha kuunga mkono kampeni hiyo.
Jumla ya vilabu tisa vinatarajiwa kuwa nyumbani siku ya Boxing day timu kama Man City na West Ham japo ombi lao limekataliwa.