Baada ya tamko la Serikali kupitia kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa kuzuia mijumuiko yote isiyo ya lazima ili kujikinga na maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona,wachezaji na Viongozi wa timu ya Namungo FC ya Ruangwa inayotumia uwanja wa Majaliwa wametimka Ruangwa na kuja bongo kumalizia mapumziko ya muda.
Kocha Mkuu wa Namungo FC,Hitimana Thiery amesema kuwa wachezaji wote wameondoka Ruangwa na kuibukia bongo ili kuchukua tahadhari ya Corona.
“Niliondoka na wachezaji kutoka Ruangwa lengo ikiwa ni kutumia wakati huu wa kupambana na virusi vya Corona, kila mmoja kuwa sehemu ambayo ni salama zaidi na wengi wamechagua kutulia Bongo na wamepewa tahadhari kwani virusi hivi sio kitu cha kuchukulia utani”alisema Thiery