Klabu ya Manchester United (Red Devil) imewataka nyota wake waliopo nje ya England kurejea haraka ndani ya siku saba ili kuendelea na majukumu yao kama zamani.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya klabu za Premier League kuanza mazoezi ili kujiandaa kwa ligi hiyo iliyosimama tangu Machi, mwaka huu kutokana na uwepo wa maambukizi ya virusi visababishwavyo na Corona.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Baadhi ya nyota wa timu hiyo ambao wapo nje ya England ni Fred (Brazil), Victor Lindelof (Sweden) na Sergio Romero (Argentina) na wengine waliotoka nje ya England wameombwa kutekeleza mamlaka hayo ili kuanza mazoezi ya ligi.