Wachezaji wa Manchester United ,Aaron Wan Bissaka na Timothy Fosu Mensah jumatatu ya wiki hii walitimuliwa na wafanyakazi wa shule St.Ambrose huko cheshire,Manchester baada ya kukutwa wakifanya mazoezi katika uwanja wa shule hiyo bila ruhusa.
Wachezaji hao walikuwa wakifanya mazoezi kwa kuzingatia sheria ya kupeana umbali lakini hata hivyo walijikuta wakiondolewa kwenye viwanja vya shule hiyo binafsi kwani hawakuwa na kibali maalum(ruhusa).
Ligi kuu ya England inatarajiwa kurejea mwezi Juni mosi licha ya wachezaji na viongozi kupinga mpango huo wa kurejea wakidai kuwa ligi irejee pale mambo yote yatakapokuwa shwari kwa kuisha kwa gonjwa la Corona kwani limekuwa tishio la dunia nzima.