Wamejileta wenyewe,Ndio msemo unaotamba hivi sasa mjini kuelekea mchezo wa fainali kombe la mapinduzi baina ya watani wa jadi Simba sc dhidi ya Yanga sc utakaofanyika kesho januari 13 katika uwanja wa Amaani mjini Zanzibar.
Yanga sc walitangulia fainali baada ya kuifunga Azam Fc mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penati huku Simba sc wakiifunga Namungo Fc mabao 2-1.
Mchezo huo unatajwa tayari umeleta presha nchini kufuatia baadhi ya mastaa waliokua mapumziko na kwenye kambi ya timu ya taifa kuanza kuzungumzwa kurejea kambini kuungana na timu visiwani humo japo inaonekana kwa wale walioko kambini na taifa stars ni ngumu kujumuika na timu hizo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.