Ikiwa tayari wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kwa alama sita baada ya kushuka uwanjani mara mbili imebainika kwamba kocha mkuu wa timu hiyo Roberto Oliveira ‘Robertinho’ yupo kwenye mipango ya kufyeka wachezaji watatu kabla dirisha la usajili halijafungwa Agosti 31.
Taarifa za ndani yaklanu hiyo zinasema kuwa wachezaji ambao wameshindwa kulishawishi benchi la ufundi na sasa uongozi unafikiria kuwatoa kwa mkopo ama ikishindikana kuwauza kabla dirisha la usajili halijafungwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na hilo mastaa kama Jimyson Mwanuke, kipa Ahmed Feruz na mshambuliaji Mohamed Mussa wapo katika hatihati ya kuwekwa sokoni kwa sasa kutokana na mapendekezo ya kocha Robertinho.