Kocha mchezaji wa Derby County inayoshiriki ligi daraja la kwanza England (championship) Wayne Rooney alionekana juzi akiendesha gari kwa mara ya kwanza baaada ya kufungiwa na mahakama kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa mwaka 2017.
Tajiri huyo mwenye magari ya kifahari ya kila aina kama LandRover Overfinch lenye thamani ya pauni 219,00 sawa na sh milioni 656 hakuwa na uwezo wa kuendesha gari kwa miaka miwili licha ya kujaza ndinga kibao nyumbani kwake.
Rooney ametoka Marekani ambako alikuwa anacheza DC United na kutua Derby kutokana na mkewe kutaka kuokoa ndoa yao baada ya mwanassoka huyo kupigwa picha akitoka hotelini Vancouver akiwa na mrembo.