Kungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso Yacouba Songne ameifungulia mashtaka kwa shirikisho la soka nchini (TFF) klabu yake ya Tabora United kisa madai ya mishahara anayodai ya miezi 4 pamoja pesa ya usajili iliyosalia kwenye usajili wake.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga sc kwa sasa ameanza mazoezi akitokea katika kipindi kirefu cha kuuguza jeraha lake la mguu ambapo amefikia uamuzi huo baada ya kukiri kutoona dalili za kulipwa stahiki zake.
Yacouba alijiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya Arta Solar ya nchini Djibouti ambayo alijiunga nayo akitokea katika kipindi kigumu cha majeraha baada ya kuachwa na Yanga sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo pamoja na kuanza vizuri msimu huu akifunga mabao muhimu kwa klabu yake Mshambuliaji huyo mwenye kasi aliumia na kulazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akitibu majeraha hasa baada ya kifanyiwa upasuaji nje ya nchi.