Mshambuliaji Yacouba Songne amepona na Sasa yuko fiti kuanza kukitumikia kikosi cha Timu ya Wananchi kuanzia michezo ijayo.
Daktari wa timu, Nahumu Muganda amesema pamoja na Yacouba, beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na kipa Ramadhan Kabwili nao wamepona na wamerejea kikosi.
“Yacouba tayari ameshapona na ameshaanza mazoezi na timu, tutakaporejea kambini kesho atakuwa tayari kutumika kadri Kocha atakavyoona inafaa kikosini,” amesema Dkt. Muganda.
Amesema Ninja na Kabwili pia wameshapona na wameanza mazoezi ya pamoja timu na wao wako tayari kutumika hivyo kuingiza idadi ya majeruhi kwenye kikosi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Tulikuwa na majeruhi saba, ukijumusia Mukoko lakini Mukoko naye yuko sawa na amenieleza kwamba kesho atarudi kambini na wenzake, hivyo tutabaki na majeruhi watatu ambao ni Said Ntibazonkiza, Dickson Job na Balama Mapinduzi,” Amesema Dkt. Muganda.