Site icon Sports Leo

Yanga Bingwa Mapinduzi 2021

Klabu ya Yanga sc imeibuka mabingwa katika kombe la mapinduzi Cup 2021 visiwani Zanzibar baada ya kuifunga timu ya Simba sc katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Amaan.

Dakika 90 za mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua huku ukiwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi zilimalizika bila kufungana huku Simba sc ikiwa haijalenga lango la Yanga hata mara moja.

Changamoto ya mikwaju ya penati iliipatia Yanga sc ubingwa baada ya kufunga penati 4 dhidi ya 3 za Simba sc huku mastaa Meddie Kagere na Joash Onyango wakikosa penati zao na Mukoko Tonombe akikosa kwa upande wa Yanga sc.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu wamejinyakulia kiasi cha Tsh milioni 15 huku Simba sc wakipata shilingi milioni 10.

Exit mobile version