Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Dodoma Jiji Fc baada ya kuifunga kwa mabao 5-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaani Visiwani Zanzibar.
Yanga sc ilianza kuandika bao la mapema dakika ya 4 kupitia kwa Cletous Chama aliyepokea pasi nzuri kutoka kwa Clement Mzize ambaye aliwatoka mabeki wa Dodoma Jiji kiufundi.
Hata hivyo muundo mzuri wa ulinzi wa Dodoma Jiji uliwafanya Yanga sc kusubiri mpaka dakika ya 52 kupata bao la pili kupitia kwa Duke Abuya aliyepokea pasi kutoka kwa Chama.
Ibrahim Hamad Bacca alifunga bao lake la tano katika ligi kuu ya Nbc nchini dakika ya 62 ya mchezo akimalizia pasi ya Maxi Nzengeli iliyokua inatoka nje ya uwanja huku Joash Onyango akijifunga dakika ya 90+2′ ya mchezo wakati akiokoa krosi ya Farid Mussa.
Dakika ya mwisho ya nyongeza ya mwamuzi Abdalah Mwinyichui kutoka Tanga baada ya Maxi Nzengeli kufunga bao la tano katika mchezo huo na kuihakikishia Yanga sc ushindi na kubeba alama tatu muhimu.
Sasa Yanga sc imefikisha alama 78 kileleni mwa msimamo ikisubiri kuifunga Simba sc ama kupata sare katika mchezo wa juni 25 2025.