Site icon Sports Leo

Yanga sc Yafungukia Ujio wa Migne

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dk.Mshindo Msolla na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya Gsm Eng.Hersi Said wakisaini Mkataba wa Ushirikiano na Kampuni ya La liga jana jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindao Yanga, amesema wanaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya atakayerithi mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze

Kumekuwa na tetesi kumuhusu kocha wa zamani wa Harambee Stars na Guinea ya Ikweta Sebastian Migne anayetajwa kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria

Hersi amesema Migne ni miongoni mwa makocha wanaofanya nao mazungumzo lakini bado hawajafikia mwafaka

“Ni kweli, Migne ni miongoni mwa makocha ambao tuko katika mazungumzo nao, lakini hayuko peke yake, wengine wapo pia. Bado mwafaka haujafikiwa kuamua yupi tumkabidhi timu, “alisema Hersi

Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kumuachia timu kocha Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu

Hata hivyo wamebadili ‘gia angani’ wakiamua kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi na Mwambusi ili hata pale ligi itakapomalizika atakuwa amefahamu uimara na madhaifu ya timu yako wapi ili imsaidie katika kufanya maboresho

Exit mobile version