Taarifa kutoka Yanga sc zinaeleza kwamba mazungumzo na Kocha Rulani Mokwena kujiunga na klabu hiyo yanaendelea vizuri ambapo kocha huyo ametoa masharti mbalimbali ili kukubali kujiunga na klabu hiyo.
Hata hivyo pamoja na kukubali huko changamoto kubwa ni kwamba Mokwena ana ofa tofauti zimeendelea kumfuata tangu aachane na Wydad Athletic Club huku ofa hizo zikiwa ni kubwa kuliko ya Yanga sc.
Katika moja ya masharti yake kocha huyo anataka mambo machache ya kuboreshwa ikiwemo kutanua benchi la ufundi na kusajiliwa wachezaji anaowataka masharti ambayo mabingwa hao wa kihistoria nchini wanapambana nayo.
Hata hivyo mastaa ambao anawataka Mokwena wengi ni wale wa bei iliyochangamka sokoni ambapo pia mahitaji yao ya mishahara ikiwa ni mikubwa kiasi ambacho klabu hiyo inaweza ishindwe kuhimili.
Pamoja na hayo pia klabu hiyo italazimika kupambana kuwabakisha kikosini wakina Pacome Zouzoua,Djigui Diarra na Clement Mzize ambaye yupo mguu mmoja nje mpaka sasa.