Home Soka Yanga Sc Yamtambulisha Abuya

Yanga Sc Yamtambulisha Abuya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha mchezaji Duke Abuya kama usajili mpya wa klabu hiyo akitokea Singida Black Stars ambayo alikua amemaliza mkataba nayo na kusaini kuichezea Yanga sc kwa msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Abuya ni kiungo mshambuliaji akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zote za kiungo wa juu ambapo amedumu Singida Black Stars kwa misimu miwili akijiunga nao akitokea Polisi Fc ya nchini Kenya ambapo alijiunga akitokea Nkana Fc ya Zambia.

Abuya atakua na changamoto ya kugombea nafasi mbele ya Stephane Azizi Ki,Maxi Nzengeli,Pacome Zouzoua na Cletous Chama ambao wote ni wazuri katika eneo la kiungo cha ushambuliaji huku wakiwa wameshafanikiwa kuonyesha uwezo wao nchini.

banner

Mchezaji huyo anaungana na Cletous Chama,Aboubakari Khomeiny,Prince Dube,Chadrack Boka kama usajili mpya mpaka sasa klabuni hapo ambao wamekuja kuongeza makali katika kikosi cha Miguel Gamondi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited