Ni rasmi sasa klabu ya Yanga sc imemuuza kiungo mshambuliaji wake Stephan Aziz Ki kwenda katika klabu ya Wydad Athletic ya nchini Morocco kwa dau linalokadiriwa zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania.
Baada ya tetesi na taarifa za awali kuhusu uwepo wa dili hilo sasa rasmi klabu hiyo imethibitisha kupitia mitandao yake ya kijamii kuachana na staa huyo na kuvuta mkwanja mrefu.
Yanga sc imechapisha maudhui maalumu ya kumuaga staa hiyo aliyeichezea klabu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo akitwaa mataji ya ligi kuu mara mbili na kombe la Shirikisho la Crdb mara tatu na kombe la ngao ya jamii mara tatu pia.
Azizi Ki tayari ameshaondoka klabuni hapo kujiunga na waajiri wake wapya nchini Morocco ambapo moja kwa moja ataingia kambini kujiandaa na michuano maalumu ya klabu bingwa duniani kwa ngazi ya vilabu itakayofanyika mwezi