Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kutwaa kombe la Muungano nchini baada ya kuifunga klabu ya Jku kwa 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika viwanja vya Gombani Visiwani Pemba.
Yanga sc ikichanganya kikosi chake cha wanaoanza mara kwa mara na wale wanaoanzia benchi kama Farid Mussa na wengine ilitawala mchezo huo muda mwingi huku Jku wakijilinda zaidi katika dakika zote za mchezo huo.
Â
Bao pekee la Maxi Nzengeli dakika ya 44 ya mchezo huo akipokea pasi nzuri ya Farid Mussa na kuutupia mpira wavuni na kusababisha shangwe kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika tisini za mwamuzi na wananchi kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo iliyorejea baada ya kusimama kwa muda mrefu.
Kombe hilo sasa ni la tatu kwa Yanga sc msimu huu baada ya kutwaa ngao ya jamii mwanzoni mwa msimu huu wakiifunga Azam Fc mabao 4-1.