Home Makala Yanga Sc Yawasili Ruangwa Kuivaa Namungo Fc

Yanga Sc Yawasili Ruangwa Kuivaa Namungo Fc

by Sports Leo
0 comments

Msafara wa mastaa wa klabu ya Yanga sc umewasili salama wilayani Ruangwa mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa Complex wilayani humo.

Asubuhi na mapema ya leo kikosi hicho kilisafiri kwa ndege mpaka Mtwara kisha Basi la klabu hiyo kuwachukua mpaka wilayani Ruangwa kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na kila timu kutaka alama tatu muhimu.

Yanga sc ikiwa haijapata ushindi katika michezo yake miwili ya ligi kuu itakutana na Namungo Fc ambayo nayo haijapata ushindi katika michezo takribani nane ya ligi kuu nchini.

banner

Ugumu mwingine wa mchezo huo ni uwepo wa kocha Juma Mgunda ambaye ni mzoefu na mwenye maarifa ya kutosha kuvaana na Yanga sc.

Namungo mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama tisa pekee katika michezo 11 ya ligi kuu huku Yanga sc wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 24 wakicheza michezo 10 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited