Site icon Sports Leo

Yanga Yatoa Msaada Kwa Mama Anna

Klabu ya Yanga kupitia kwa mdhamini wao kampuni ya GSM jana Januari 30,20 wamefanikisha kutoa masaada wa fedha na mahitaji ya chakula cha miezi mitatu pamoja na gharama ya matibabu ya Anna Majaliwa.

Yanga imetoa  msaada huo kwenye familia ya Anna ambaye anasumbuliwa na tatizo la mwili kukosa fahamu ndani ya miaka mitatu jambo lililompelekea kushindwa kupata choo kwa zaidi ya miezi sita.

Akizungumza Anna alisema kuwa alipata tatizo hilo kwa zaidi ya miaka hiyo mitatu jambo linalomfanya kupata tabu kila kukicha hivyo anawashukuru sana Yanga kupitia mdhamini wao GSM kwa kutambua tatizo lake.

“Najisiki faraja sana kuiona timu yangu Yanga kupitia kwa mdhamini GSM ambao kwa namna kubwa wametambua tatizo langu na kujitolea msada huu wa chakula pamoja na godoro ambalo kiukweli sikuwa nalo nasikuwa na uwezo wa kununua”alisema mama Anna
Kwa upande wa Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa mbali na misaada iliyotoleo jana pia GSM itahakikisha inampatia matatibabu Anna hata nje ya nchi huku ikimhudumia chakula kwa muda wa miezi mitatu.

 

Exit mobile version