Home Soka Yusufu Kagoma Atua Simba Sc

Yusufu Kagoma Atua Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Baada ya tetesi kuwa amesaini timu mbili,Hatimaye klabu ya Simba Sc imemtambulisha rasmi kiungo Yussufu Kagoma kama mchezaji mpya wa timu hiyo ikimsajili kutoka Singida Fountain Gate Fc ambapo sasa atakua mchezaji wa 12 kutambulishwa na timu hiyo.

Simba sc imetambulisha Kagoma baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kujiunga na kikosi hicho ili kurejesha ufalme wake uliopotea kwa takribani miaka mitatu sasa bila kutwaa taji lolote la maana zaidi ya kujiliwaza na taji la ngao ya jamii na kombe la Muungano.

Awali Kagoma aliripotiwa kuwa amesaini Yanga sc lakini baada ya kupata ofa ya Simba Sc inasemekana mchezaji huyo ilimvutia zaidi na kuanza taratibu za kumalizana na Yanga sc kwa kurejesha fedha kisha kujiunga na Simba Sc ambapo anaona atakua na furaha zaidi.

banner

Uwepo wa Khalid Aucho katika kiungo cha chini cha ukabaji cha Yanga sc inatajwa ni moja ya sababu ya staa huyo kubadili mawazo na kuamua kujiunga na Simba sc kwa hofu ya kukosa namba.

Kagoma amewahi kuzichezea timu za Geita Gold Sc sambamba na klabu ya Singida Fountain Gate Fc ambapo alikua na mgogoro na klabu hiyo tangu mwezi Januari alipoamua kuondoka kambini mpaka Simba Sc ilipoamua kununua mkataba wake klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited