Site icon Sports Leo

Azam Fc Yanasa Kocha Msenegali

Klabu ya Azam Fc imemtangaza Youssouph Dabo kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao wa 2023/2024 akisaini mkataba wa miaka mitatu na kutambulishwa kwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

Dabo raia wa Senegal anachukua nafasi ya Dennis Lavagne aliyetimuliwa klabuni hapo miezi kadhaa iliyopita kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu klabuni hapo licha ya mabosi wa klabu hiyo kufanya usajili wa mastaa wa maana.

Kocha huyo amewahi kuvifundisha vilabu vya Sans Club,Asc Jaraaf,Teungueth Fc na kikosi cha timu ya Taifa ya Senegal chini ya miaka 20 anakuja Azam Fc kujaribu kuipa ushindani timu hiyo ambayo ilianza msimu vizuri lakini mwishoni imekua na matokeo mabovu kiasi cha kutolewa kwenye michuano ya kimataifa na katika mbio za ligi kuu nchini.

Exit mobile version