Bondia raia wa Tanzania Kennedy Ayo amekwama nchini Urusi baada ya kukosa nauli ya kurudi nyumbani kutokana na ubabaishaji wa promota wa pambano lake nchini humo.
Bondia huyo alikwenda kupambana dhidi ya Bondia aliyefahamika kwa jina la Guliyev na kufanikiwa kupata ushindi kwa pointi kutoka kwa majaji wote watatu.
Baada ya pambano hilo bondia huyo alipata changamoto ya tiketi ambapo promota wa pambano hilo alimwambia akate tiketi kwa gharama zake baada ya ile ya awali kuleta matatizo.
Gharama za tiketi kutoka nchini humo mpaka hapa inakadiriwa kufikia dola 1000 za marekani huku bondia huyo akiwa nv kiasi cha dola 800 pekee.
Tayari mamlaka za ngumi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Sanaa na Michezo kupitia ubalozi wa Tanzania nchini humo zimeanza harakati za kutatua suala hilo.