Bondia wa Mexico Carnelo Alvarez amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Unidisputed world super middleweight championships baada ya kumchapa kwa TKO bondia Caleb Plant usiku wa kuamkia leo.
Pambano hilo lilifanyika huko Las Vegas Marekani katika ukumbi maarufu wa MGM Arena lilishuhudia bondia huyo akimwangusha Mmarekani Caleb mara mbili katika raudi ya 11 na kumaliza mchezo.
Canelo anakuwa bondia wa kwanza kwenye historia ya masumbwi kumiliki mikanda yote ya uzito wa kati.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bondia huyo anayetokea katika kambi ya Floyd Maywether ameshinda jumla ya mapambano 57 akitoa sare mawili na kupigwa moja tu tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa.
Mabondia wa zamani Mike Tyson na Manny Pacquiao wamemsifu na kumpongeza Canelo kwa kusema alikuwa mkali zaidi ya mpinzani wake na kwamba masumbwi yako salama mikononi mwake.