Sports Leo

25 waitwa Taifa Stars kuwavaa Benin

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 25 watakaojiunga na timu hiyo kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu kombe la dunia Qatar 2022 dhidi ya Benin

Kikosi hicho hakina mabadiliko sana na kile kilichocheza michezo miwili ya kwanza dhidi ya DR Congo na Madagascar,wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ni Jonas Mkude na John Bocco ambaye alikosa michezo ya mwanzo kutokana na majeruhi.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Benin ugenini kabla ya kurudiana nao tena katika mchezo wa nne jijini Dar es salaam katika kalenda ya FIFA inatarajiwa kuanza tena Oktoba 5 mwaka huu.

Kikosi kamili ni kama ifuatavyo.

Exit mobile version