Home Soka Al Ahly Wawasili Usiku

Al Ahly Wawasili Usiku

by Sports Leo
0 comments

Msafara wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri kimewasili nchini machi 27 wa kuamkia leo kikiwa na mahitaji yote muhimu ikiwemo chakula na maji kwa ajili ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baina ya timu hiyo na Simba sc.

Msafara huo ambao awali ulitanguliwa na maofisa wa klabu hiyo waliokuja mapema kuandaa mazingira uliwasili mida ya jioni machi 27 na kuelekea moja kwa moja hotelini ambapo jana usiku walifanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana katikati ya jiji la Dar es salaam.

banner

Simba sc na Al Ahly zitakutana siku ya ijumaa machi 29 saa tatu usiku katika mchezo wa kwanza ambao utafanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambapo kutokana na presha na ugumu wa mchezo huo imewalazimu Al Ahly kuja nchini na Vyakula na Maji ya kunywa wakiogopa fitna.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika ufunguzi wa michuano ya African Football league ambapo mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam timu hizo zilitoka sare ya 2-2 na mchezo wa marudiano jijini Cairo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na Simba Sc kuaga mashindano hayo yaliyokua yanafanyika kwa mara ya kwanza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited