Site icon Sports Leo

Allegri Kumrithi Pirlo Juve

Klabu ya Juventus ipo mbioni kumtangaza kocha Massimiliano Allegri kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya Andrea Pirlo baada ya kutoridhishwa na ufanisi wake hasa baada ya kukosa ndoo ya ubingwa wa Serie A.

Pirlo licha ya kuwa na kikosi cha mastaa wa maana akiwemo Cristiano Ronaldo ameshindwa kuipa timu hiyo taji la 10 mfululizo kiasi cha kuishia kufuzu Uefa pekee.

Allegri 53′ amekua hana timu tangu mwaka 2019 alipoondoka Juve na nafasi yake kuchukuliwa na Maurizio Sarri ambaye naye hakudumu na kumuachia Pirlo ambaye ameshindwa kuifanya timu hiyo kuwa tishio katika msimu wake wa kwanza.

Exit mobile version