Site icon Sports Leo

Argentina bingwa Copa America

Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa Amerika ya Kusini baada ya kuwafungwa wapinzani wao wakubwa timu ya Taifa ya Brazil kwa bao moja kwa bila.

Argentina ilijipatia bao lake dakika ya 22 ya mchezo kupitia kwa Angel Di Maria akipokea pasi safi ya Rodrigo De Paul, na kuamsha shangwe za mashabiki wa taifa hilo waliohudhuria fainali hiyo iliyofanyika katika dimba la Maracana nchini Brazil.

Taji hilo litamfuta machozi nyota wa taifa hilo Lionel Messi ambaye amekuwa akikosolewa na Waargentina kwa kushindwa kulipa taji kama anavyofanya akiwa katika klabu yake ya Barcelona.

Hii ni mara ya kwanza kwa Argentina kutwaa taji lolote kubwa toka mwaka 1993.

Exit mobile version