Klabu ya arsenal ya Uingereza yakubali kuongeza dau la usajili la mlinzi wa kati wa kati wa Brighton and Hove Albion Ben White raia wa Uingereza mwenye miaka 23 hadi kufikia kiasi cha paundi 50m baada ya ofa yao ya awali ya paundi 40m kukataliwa na Brighton wiki iliyopita.
Beki huyo wa kati mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani amekuwa akiwindwa na klabu ya arsenal katika dirisha hili kurithi mikoba ya Mbrazil David Luiz aliyeondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu uliopita.
White amejumuishwa na kocha Gareth Southgate wa timu ya taifa kuchukua nafasi ya beki wa Liverpool Alexander Anold aliyeumia ili kuiongezea nguvu Uingereza katika michuano inayoendelea ya Euro 2020 .