Home Soka Azam Fc Vs Yanga sc Kufanyika B/mkapa

Azam Fc Vs Yanga sc Kufanyika B/mkapa

by Sports Leo
0 comments

Serikali kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo imekubali ombi la klabu ya Azam Fc kutumia uwanja wa Benjamini Mkapa katika michezo yake miwili ya ligi kuu dhidi ya Yanga sc na Simba sc ambapo klabu hiyo itakua mwenyeji wa michezo hiyo.

Azam Fc imekua ikitumia uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam lakini kutokana na ukubwa wa michezo hiyo miwili ambayo huvutia mashabiki wengi umeifanya klabu hiyo kuomba kutumia uwanja huo mkubwa wenye uwezo wa kuingiza watazamaji elfu sitini ambao umesimamishwa na serikali kutumika kutokana na kufanyiwa ukarabati mkubwa ambapo michuano ya kimataifa pekee ndio ilikua inaruhusiwa kufanyika uwanjani hapo.

Mchezo baina ya klabu hiyo na Yanga sc unatarajiwa kufanyika machi 17 katika uwanja huo ambapo mpaka sasa tayari tambo zimeanza kutokana na vikosi vyote kuwa katika viwango bora na vikiwa na mastaa mahiri kabisa wakiwemo James Akaminko,Feisal Salum ambao watakua na kazi ya kupambana na Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua.

banner

Katika msimamo wa ligi kuu nchini Yanga sc wapo kileleni wakiwa na alama 49 katika michezo 18 ya ligi kuu huku Azam Fc wakiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na alama 44 katika michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc ambapo endapo Yanga sc atashinda mchezo huo basi atakua amejihakikishia nafasi kubwa ya kuwa mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited