Klabu ya Azam fc imeendelea kuipigania nafasi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara baada ya jana kuifunga timu ya Mbao fc mabao 2-0 na kuendelea kusalia nafasi ya pili ya Msimamo.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex,Mabao ya Azam FC yalifungwa na Richard Djod dakika ya 49 kwa pasi ya Idd Naldo huku lile la pili likifungwa na Idd Chilunda dakika ya 90+3.
Mbao baada ya kupoteza mchezo huo unawafanya wasalie nafasi ya 19 ikiwa na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 30 huku Azam wakibaki nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 29.