Sports Leo

Azam FC yaanza kwa sare TPL,Namungo kileleni

Waoka mikate wa Chamazi Azam Fc imeanza ligi kuu Tanzania Bara kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union katika mchezo uliofanyika katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Azam walijipatia goli lake dakika ya 48 kipindi cha pili kupitia kwa beki Daniel Amoah akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Idd Suleiman.Zikiwa zimesalia dakika chache kutamatika kwa mchezo huo beki Hance aliisawazishia Coastal na kubakiza alama moja katika uwanja wa nyumbani.

Sare hiyo imeendeleza rekodi ya Coastal Union kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Azam wakiwa Mkwakwani.

       

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mchana Mbeya Kwanza wameiduwaza Mtibwa Sugar kwa ushindi wa 1-0 katika dimba la Mabatini Ruvu huku Wauaji wa Kusini  Namungo wakiichabanga Geita Gold kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Shiza Kichuya na Reliant Lusajo.

Ligi hiyo itaendelea hapo kesho ambapo mabingwa watetezi Simba itakuwa Mara kukabiliana na Biashara United katika uwanja wa Karume.

Exit mobile version