Klabu ya soka ya Azam imekamilisha usajili wa mshambuliaji hatari toka klabu ya Zanaco ya Zambia Rodgers Kola kwa mkataba wa miaka miwili hadi 2023.
Mzambia huyo aliifungia Zanaco fc magoli 12 katika ligi kuu ya zambia akiwa nyuma ya mshambuliaje mwenzake Zanaco Moses Phiri aliyeifunga magoli 17. mchezaji huyo pia alikuwa akihusishwa na vilabu kadhaa vya Afrika Kusini kabla ya kutua kwa matajiri hao wa jiji la Dar es salaam.
Usajili huo ni muendelezo wa Azam fc kujijenga zaidi ili kushindani na vilabu vikubwa vya Simba na Yanga pamoja na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya ule wa awali wa kiungo mwengine Mzambia Charles Zulu.