Site icon Sports Leo

Azam Haoo Nusu Fainali

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la Azam baada ya kuifunga klabu ya Rhino Rangers ya Tabora kwa mabao 3-1.

Seleman Abdalah alipachika bao kwa Rhino Rangers dakika ya 31 lakini bao hilo lilidumu kwa dakika mbili tu ambapo  Ayoub Lyanga alisawazisha,huku mabao mengine ya Azam FC yalifungwa na  Agreý Morris 65′ na Obrey Chirwa 80′.

Sasa Azam Fc inasubiri mshindi kati ya Simba sc na Dodoma Jiji Fc ili kujua itakayekutana nae nusu fainali.

Exit mobile version