Site icon Sports Leo

Barca vs Bayern hapatoshi UEFA

Klabu ya soka ya Barcelona inatarajia kumenyana na mabingwa wa soka Ujerumani Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa kundi E katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA.

Miamba hiyo ya soka itacheza mchezo huo katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana hatua ya robo fainali mwaka 2020 ambapo Bayern waliibuka na ushindi wa mabao 8-2.hivyo mechi hiyo ni kama ya kisasi kwa Barca ambao kikosi chao hakitishii sana baada ya kuondoka kwa Lionel Messi na Antoine Giezmann.

Jumla ya mechi 8 zinatarajiwa kupigwa hii leo,michezo mingine ni;

1.Young Boys vs Manchester United (saa 1:45 usiku)

2.Dynamo Kyiv vs Benfica (saa 4:00 usiku)

3.Villareal vs Atalanta (saa 4:00 usiku)

4.Chelsea vs Zenit St Petersburg (saa 4:00 usiku)

5.Malmo vs Juventus (saa 4:00 usiku)

6.Sevilla vs Salzburg (saa 1:45 usiku)

7.Lille vs Wolfsburg (saa 4:00 usiku).

Exit mobile version