Home Soka Bocco Ahamia Ukocha

Bocco Ahamia Ukocha

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, John Raphael Bocco ameanza kusomea ukocha wa ngazi ya awali zinazoendeshwa na TFF Makao Makuu Karume ikiwa ni miezi michache kabla ya Mkataba wake na Simba kumalizika mwishoni mwa Msimu huu.

Bocco mwenye umri wa Miaka 34 amekuwa na wakati mgumu ndani ya Simba baada ya kupoteza nafasi ya kucheza kwa misimu miwili ambapo mastaa wa kigeni wamechukua hatamu katika nafasi ya ushambuliaji kikosini humo.

Ikiwa tayari mkataba wake unaelekea kuisha Taarifa zinasema huenda akatangaza kustaafu kucheza mwishoni mwa msimu huu na moja kwa moja ana mpango wa kujikita zaidi kwenye ukocha.

banner

Bocco mshambuliaji aliyeibuka akiwa Azam Fc ambapo alitengeneza jina akiwa na klabu hiyo aliyohudumu kuanzia mwaka 2007 mpaka 2018 kisha kuhamia Simba sc ambapo pia alifanya vizuri takribani misimu kadhaa ya mwanzoni kabla ya kupoteza nafasi kikosini humo.

Msimu huu Simba sc imewasajili Pa Omar Jobe na Fredy Michael katika eneo la ushambuliaji ambapo kocha Abdelhack Benchika anapendelea kuwatumia mara kwa mara pamoja na Kibu Dennis.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited