Home Soka Bocco Apelekwa Timu ya Vijana

Bocco Apelekwa Timu ya Vijana

by Sports Leo
0 comments

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema klabu hiyo imemtoa mshambuliaji wake John Bocco kutoka kuwa nahodha wa timu hiyo na sasa anafundisha timu ya vijana ya klabu hiyo kama kocha mkuu.

Kajula aliyasema hayo Bungeni Dodoma wakati alipohudhuria vikao vya Bunge kama mgeni mwaliko huku pia akiwa mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi wa Simba Executive Network yenye lengo la kuimarisha uongozi wa klabu hiyo.

Kajula alisema kuwa wao kama klabu wanaamini katika kumuendeleza mchezaji baada ya muda wake wa kucheza kuelekea mwishoni huku pia akisema kuwa suala hilo pia limekua na tija kwa mchezaji huo na klabu kwa ujumla.

banner

Klabu ya Simba sc kwa takribani misimu mitatu sasa imeshindwa kufanya vizuri pamoja na mabadiliko kadhaa hasa ndani ya uwanja ikiwemo kubadili waalimu na wachezaji lakini mwishoni hakuna mabadiliko yeyote na sasa ina mpango mkubwa wa kubadilisha uongozi wa juu wa klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited